UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATA JIJINI NAIROBI UMETEKETEA KWA MOTO
Biashara na shughuli za kiuchumi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya zimetishwa kwa muda usiojulikana, kutokana na moto mkubwa kuzuka katika uwanja huo leo saa 11 alfajiri.Mamlaka za usalama katika uwanja mkuu wa ndege nchini Kenya zimesema safari zote za ndege katika uwanja huo zimesitishwa na wasafiri kuhamishwa.
Vikosi vya dharura kutoka jeshini, zima moto, na chama cha msalaba mwekundu katika Kaunti ya Nairobi na Kenya vinapambana kuuzima moto huo tangu alfajiri.
Hakuna taarifa zozote za majeruhi ambapo chanzo cha moto huo ulioanza majira ya saa kumi na moja alfajiri bado hakijajulikana.
Tayari kamati kuchunguza chanzo cha moto huo inayoongozwa na waziri wa uchukuzi wa Kenya Mhandisi Michel Kamau imeundwa.
Mpaka sasa hakuna ndege inayoruhusiwa kutua wala kuondoka ambapo ndege zote zimeelekezwa kutua katika Uwanja wa ndege wa Mombasa, Eldoret na Dar es salaam.