UNAMKUBALI 50 CENT. HICHI NDIO KITABU CHAKE KIPYA CHA MAZOEZI.
50 cent aka Curtis Jackson ametoa kitabu cha mazoezi ya viungo chenye ratiba ya Wiki 6, Kitabu hicho kinaonyesha jinsi yakufanya mazoezi na ulaji wako wakati wa mazoezi hayo. Kitabu cha Formula 50 kinahamasishwa Na mambo aliyo pitia 50 cent wakati alipokuwa akifanya mazoezi baada ya kupigwa risasi tisa mwaka 2000.
Kitabu na ratiba yake ya wiki sita hairuhusu madawa yoyote kutumika. Kwenye litabu hichi 50 Cent anakufundisha kuwa na mwili mzuri wenye afya kama wake na mazoezi unayoweza kufanya kama ni mtu mwenye kazi sana na huna muda wa gym.Pia anakupa maelekezo jinsi ya kumudu mazingira ya gym ukiwa na msongo wa mawazo.